MADHARA YATOKANAYO NA ULAJI NGURUWE
Je ni hatari kula nguruwe? Hilo ndilo swali wanalojiuliza watu wa Madagascar baada ya utata juu ya kuwepo kwa vichocheo (homoni) hatari kwenye nyama za nguruwe.
Mwaka jana, serikali ilipiga marufuku mauzo ya kiholela ya dawa za vichocheo vya mwili , baada ya uchunguzi kufichua kwamba 87% ya nguruwe wanaouzwa sokoni wanavichocheo vya mwili vinavyotumiwa kwa ajili ya kuzuia mimba.
Maafisa nchini Madagascar wamesema kuwa wanaanzisha uchunguzi kuhusu madhara ya afya ya biadamu yanayoweza kusababishwa na dawa hizo, ambazo zimekuwa zikitumiwa tangu mwaka 2010.
Vinapotumiwa kama tiba, sindano ya vichocheo hivyo vya mwili inaweza kusababisha athari kama vile kuongezeka kwa unene, ukosefu wa raha, kuchoka kwa mwili na hufanya mifupa ya mwili kuwa dhaifu, lakini haijabainika ikiwa ulaji wa chakula chene dawa hizo unasababishahatari zozote.
Category:
0 comments