.

.

DAR INACHAKULA CHA KUTOSHA

ZePLAN | 02:19:00 | 0 comments

 Mkoa wa Dar es Salaam hauna uhaba wa chakula na wanaosambaza taarifa hizo wana lengo la kujitafutia umaarufu na kutaka kuleta taharuki jambo ambalo haliachwa litokee.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Happi amesema hayo jana kwenye ziara ya kutembelea masoko na maghala ya Serikali na ya watu binafsi yaliyopo mkoani humo.

Mkuu huyo wa wilaya ambaye aliimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesisitiza kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wafanyabiashara wote watakaobainika kusambaza taarifa potofu kwa wananchi.


“Pasiwapo na mfanyabishara yeyote atakayetumia taarifa hizi za uzushi kuficha chakula, kwasababu sisi ni Serikali, vyombo vya dola vitafuatilia na mfanyabishara atakayebainika kuficha chakula kwa makusudi ili asubiri bei zipande au chakula kiadimike, huyo ni muhujumu uchumi,” amesema kaimu mkuu wa koa wa Dar es salaam na mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh Ally Happi baada ya kufanya ziara katika masoko yaliopo jijini na kujiridhisha.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments