WATU 254 WAPOTEZA MAISHA COLOMBIA
Zoezi la uokoaji likiwa linaendelea |
Watu 254 wanaelezwa kupoteza maisha kwenye tukio hilo baya siku ya ijumaa Dimitri O' Donnell ni mwandishi wa Habari katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bogota
'' Katika kipindi cha saa tatu , asilimia 30 ya mvua ambayo hunyesha mjini Mocoa, kwa mwezi ilinyesha kwa saa hizo tatu, kiasi ambacho kingenyesha kwa siku takriban 10, kwa hiyo ilikua mvua ya kumshtua kila mtu''
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos ambaye anautembelea mji wa Mocoa kwa siku mbili sasa amesema zaidi zaidi ya watu 200 wamebainika kupoteza maisha, miongoni mwao watoto 44. idadi zaidi ya waliopoteza maisha inatarajiwa kuongezeka kwa kuwa bado watu takriban 300 bado hawajulikani walipo.
Mwanabaiolojia Carolina Pardo kutoka chuo kikuu cha El Rosario mjini Bogota,amezungumza na amesema matumizi mabaya ya ardhi yamesababisha mmomonyoko wa udongo uliosababisha maporomoko ya ardhi.
Category:
0 comments