HATARI DUNIANI JOTO LAONGEZEKA ZAIDI
Kwa kipindi cha miezi kumi na mbili,Hali ya joto duniani imefikia kiwango cha juu zaidi kilichowahi kutokea kwa miaka mitatu mfululizo.
Utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa na kusaidiwa na shirika la uchunguzi wa masuala ya anga
( NASA), umebaini kuwa wastani wa joto kabla ya mapinduzi ya viwanda ilikuwa ni kipimo cha celsius 1.1.
Madhara yanayotokana na hali hii ni pamoja na ukame huko nchini India, na kuyeyuka kwa kiwango kikubwa cha barafu katika ukanda wa Arctic.
Wataalamu wametaja sababu za kuongezeka kwa joto duniani kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu kama vile shughuli za viwanda zinazochangia kiasi kikubwa cha gesi chafu na hali ya matukio ya asili maarufu kama El Nino yanayosafirisha joto kutoka katika bahari ya pasifiki.
Huu ni mmoja kati ya miaka 16 ya joto zaidi kuwahi kutokea, hali hii imetokea tena karne hii.
Category:
0 comments