.

.

KIZAAZAA CHAIBUKA MOROGORO MABOMU YA MACHOZI YARINDIMA

ZePLAN | 23:37:00 | 0 comments

Polisi mjini Morogoro  wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chadema baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni katika Kata ya Kiwanja cha Ndege.

Kabla ya kurusha mabomu hayo saa 12:30 jioni, dereva wa gari la matangazo lililotumika katika kampeni hizo aliamriwa kuzima muziki huku wafuasi hao wakitakiwa kurudi nyumbani bila ya kufanya maandamano ambayo yanaweza kuhatarisha usalama.

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Morogoro (OCD), Peter Nsato amesema walilazimika kurusha mabomu ya machozi baada ya wafuasi wa Chadema kuandamana katika mitaa mbalimbali ya kata hiyo hali ambayo ingeweza kusababisha uvunjifu wa Amani.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments