.

.

REAL MADRID YAKUBALI KICHAPO KUTOKA KWA CELTA VIGO CHA 2-1

ZePLAN | 23:45:00 | 0 comments

Iago Aspas akisherehekea kuifunga Real Madrid


Real Madrid wameshindwa kwenye mechi ya pili mfululizo kwa mara ya kwanza tangu Novemba 2015 baada ya Celta Vigo kuwalaza 2-1 mechi ya mkondo wa kwanza robofainali ya Kombe la Mfalme, Copa del Rey..

Madrid, ambao mkimbio wao wa kutoshindwa mechi 40 ulifikishwa kikomo na Sevilla siku ya Jumapili, walijipata nyuma kwenye mechi pale mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Iago Aspas alipofunga bao lake la 16 msimu huu.

Madrid walisawazisha kupitia Marcelo lakini Jonny akawahakikishia ushindi baada ya kufunga sekunde chache baadaye kupitia kaunta kwenye mechi hiyo iliyochezewa Bernabeu.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments