.

.

JAJI MKUU ALA KIAPO MBELE YA MH RAIS IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

ZePLAN | 23:23:00 | 0 comments

Kaimu Jaji Mkuu akila kiapo mbele ya Rais wa Jamuhuri ya uungano wa Tanzania Mh John Magufuli
|
Kaimu Jaji Mkuu mpya wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma ameahidi kuweka mkazo katika matumizi ya Tehama katika kuendesha kazi za Mahakama kuhakikisha haki inapatikana kwa haraka.

Jaji Juma alitoa ahadi hiyo baada ya kuapishwa, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana.

Jaji Juma awali alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania na atashika nafasi hiyo mpaka hapo Rais Magufuli atakapofanya uteuzi wa Jaji Mkuu. “Katika kuwahudumia wananchi katika kutoa haki na kwa haraka tutatumia teknolojia ya habari ili haki iweze kupatikana haraka kuliko sasa,” alisema Jaji Juma.

 
Alisema alipata nafasi ya kusoma sera ya Tehama iliyotolewa Mei mwaka jana ambayo inatoa picha ya nchi miaka 20 ijayo kuonesha nchi inatakiwa kwenda wapi ambapo na mahakama inatakiwa kutekeleza. “Mpango wangu ni kwamba, kesi zinasajiliwa katika mtindo huo ili kuhakikisha haki inapatikana haraka na kwa uwazi zaidi ya ilivyo sasa,” alisema Jaji Juma na kuwapongeza majaji wakuu waliomtangulia ambao waliweka msingi wa mabadiliko katika mahakama ikiwa ni pamoja na kuweka mpango mkakati unaosaidia katika utendaji kazi. “Sheria nyingi zimebadilika, fedha nyingi zimepatikana na vilevile mpango mkakati wa mahakama, sasa ni kuutekeleza mpango huo ….. wao wameshamaliza kazi yao sasa ni kupunguza maneno”, alisema Jaji Juma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan  na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Profesa Sifuni Mchome na Naibu wake Mhe. Amon Mpanju wakiwa katika picha ya pamoja


Aidha alimshukuru pia Rais John Magufuli kwa kumuamini na kumteua katika nafasi hiyo ili aweze kuwahudumia wananchi katika kutoa haki. Rais Magufuli juzi alimteua Jaji Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania kuchukua nafasi ya Jaji Mohamed Chande Othman ambaye amestaafu.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments