MAN U YATOA RUKSA KWA MEMPHIS KWENDA KUFANYA VIPIMO LYON
Manchester United imemruhusu Memphis Depay kusafiri kwenda kufanya vipimo vya afya katika klabu ya Lyon.
United na Lyon wamekubaliana ada ya kwanza £16m na malipo yanaweza kufikia mpaka £21m.
Mashetani Wekundu pia wameweka vifungu vya kumnunua upya Depay kulingana na makubaliano pamoja na kupata malipo ya ziada endapo mchezaji atauzwa na Lyon kwenda klabu nyingine kwa faida.
Category:
0 comments