Toure amekuwa muhimili muhimu tokea alipojiunga na city 2010
Kiungo wa kati wa timu ya Manchester City Yaya Toure amepiga chini ofa ya dola za kimarekani 459,000 kwa wiki iliyotangazwa na China.
Toure mwenye umri wa miaka 33 angekuwa mchezaji muhimu katika ligi ya uchina inayotarajiwa kufanyika msimu ujao. Ameamua kupingana huku mkataba wa mchezaji huyo wa Ivory Coast ukitarajiwa kuisha majira ya joto.
Mustakabali wa Toure ulionekana kuwa njia baada ya kuachwa nje ya kikosi tokea mwanzo wa msimu.
Mwanzoni mwa msimu Toure ambaye amekuwa injini ya city aliwekwa benchi na kocha Guardiola
Lakini kwa sasa amekuwa akicheza mara kwa mara tokea mwezi Novemba na kuwa muhimu kwenye klabu hiyo. Toure amekuwa huru kusaini mkataba mpya na timu yoyote kutoka nje ya Uingereza lakini anakiri kuwa ana furaha kuendelea kubaki EPL.
Baada tu ya kurejea Toure alifunga magoli mawili muhimu dhidi ya Crystal Palace
Toure raia wa Ivory Coast, alijiunga na City mwaka 2010 amekuwa nguzo kwenye klabu hiyo na hivi karibuni ameonekana kuwa mustakabali wa mjerumani Ilkay Gundogan ambaye atakuwa nje ya uwanja mpaka mwisho wa msimu kutokana na majeraha.
Category:
About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!
Related posts:
If you enjoyed this article, subscribe to receive more just like it.
0 comments