CHELSEA YAIFUNGA MAN CITY MBILI MOJA HUKU ARSENAL NAE AKIIBUKA KIDEDEA ZIDI YA WEST HAM
Eden Hazard akitia kimiyani goli la kwanza la Chelsea |
Hapo jana nyasi ziliendelea kupamba moto baada ya timu mbali mbali kutimua moto katika viwanja mbalimbali huko Ulaya.
Chelsea ambao walikutana na Man city waliweza kuisambaratisha Man city kwa kifurushi cha mabao mawili kupitia winga wao mahiri Eden Hazard, huku bao la Man City la kufutia machozi likifungwa na Sergio Aguero .
Arsenal wakicheza katika uwanja wao wa Emirate waliwachapa West Ham kwa mabao 3-0 na hivyo Arsenal kurejea katika nafasi ya tano.
Theo Walcot na Mesut Ozil wakishangilia goli |
Tottenham Hotspur wakicheza ugenini katika uwanja wa Libery walitoka kidedea kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Swansea City, Southampton wakashinda kwa 3 - 1 dhidi ya Crystal Palace.
Category:
0 comments