DONALD TRUMP KUJIANDAA KUPAMBANA NA KOREA KASKAZINI
Rais wa Marekani Donald Trump |
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa Marekani itajiandaa yenyewe kuchukua hatua dhidi ya vitisho vya Nuklia vinavyoonyeshwa na Korea kaskazini.
Akihojiwa na Gazeti la Financial Times pia bwana Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter mnamo tarehe 17 ya mwezi huu , Trump amenukuliwa akisema ''kama China haitafanya chochote dhidi ya Korea kaskazini, sisi tutafanya''.
Majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliyotekelezwa na Korea kaskazini, yatawaleta ana kwa ana kwa mara ya kwanza Trump na mwenzake wa China Xi Jinping.
kabla ya mkutano wa juma hili mjini Florida, washauri wa masuala ya usalama nchini Marekani wameelezwa kuharakisha kukamilisha orodha ya sera zilizopendekezwa.
Katika ziara yake ya kwanza katika bara la Asia, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson amesema diplomasia ya miaka 20 ya nchi za magharibi iliyolenga kuidhibiti Korea kaskazini imeshindwa.
Category:
0 comments