.

.

PICHA YA NYWELE ZA ASILI ZA MKE WA RAIS MSTAAFU WA MAREKANI MICHELLE OBAMA ZAZUA GUMZO MITANDAONI

ZePLAN | 01:16:00 | 0 comments


Picha ya nywele asilia za bi Michelle Obama yazua hisia mitandaoniHaki miliki ya pich
Image captionPicha ya nywele asilia za bi Michelle Obama

Picha iliomuonyesha mke wa aliyekuwa rais wa Marekani Barrack Obama akiwa amezifunga nywele zake nyuma, badala ya alivyokuwa akitengeza nywele zake wakati akiwa mke wa kwanza wa taifa la Marekani katika kipindi cha miaka minane katika ikulu ya Whitehouse imesambazwa sana katika mitandao ya kijamii.
Ujumbe wa Twitter uliochapisha picha ya Michelle Obama umesambazwa zaidi ya mara 30,000.
Haijulikani ni lini ama wapi picha hiyo ilipigwa ,lakini mumewe Barrack Obama anaandika kumbukumbu ya wakati alipokuwa rais katika eneo la Tetiaroa, kisiwa kilichopo kusini mwa Pacific kilichomilikiwa na Marlon Brando, kulingana na gazeti la Washington Post.
Michelle Obama participates in a panel discussion at Glamour Hosts
Picha ya nywele zake kabla
Nywele zimekuwa swala la kisiasa barani Afrika miongoni mwa jamii za watu weusi.
Mwandishi wa vitabu nchini Nigeria Chimamanda Ngozi Adichie amesema kuwa iwapo Bi Michelle Obama alikuwa na nywele asili, Barrack Obama asingeebuka mshindi.
Kemikali za nywele ambazo hunyorosha nywele zimekuwa na umaarufu kwa miaka mingi.
Lakini huku mbinu hiyo ya kuweka nyewle ikionekana kuwa ya kitaalam ,wengine wanasema sio ya Kiafrika.
''Kunyorosha nyewle ni sawa na kuwa jela, bi Adichie aliandika. Ni kama mfungwa. Nywele zako zinakutawala''.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments