KUMI WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA BAADA YA KUZAMA KWA CHOMBO CHAO CHA USAFIRI ZANZIBAR
Baada ya habari ya msichana wa miaka 16 kujirusha baharini kutoka kwenye boti ya abiria iliokuwa ikifanya safari zake kutoka Dar es salaam kwenda Unguja kwa boti ya Azam na kuzua gumzo nchini Tanzania.
Leo inasadikiwa takriban watu 10 wanahofiwa kufa maji baada ya boti iliyokuwa imebeba watu takriban 50 kuzama baharini, visiwani Zanzibar.
Habari zilizowasilishwa mara baada ya kuzungumza na nahodha wa boti ya Azam SeaLink inayosafiri kutoka kisiwa cha Pemba kwenda kisiwa cha Unguja Nassor Aboubakar, waliofanikiwa kumuokoa mmoja wa wavuvi hao.
Usafiri wa namna hii umekuwa ukitumika sana kitu ambacho imekuwa ikihatarisha sana maisha ya watu kutokana na vyombo vitumikavyo kutokuwa na ubora na viwango vya kutosha kwa ajili ya kusafirishia abiria.
Category:
0 comments