CHELSEA YASHINDA ,DIEGO COSTA AJERUHIWA
Mkufunzi wa kilabu ya Chelsea Jose Mourinho
amesema kuwa ilikuwa hatari kumchezesha
mshambuliaji Diego Costa baada ya kujeruhiwa
wakati wa ushindi wa Chelsea wa 2-1 dhidi ya
kilabu ya Stoke City siku ya jumamosi.
Costa alichukua mahala pake Oscar wakati wa
mapumziko huku mabao yakiwa 1-1, lakini
alicheza kwa dakika 10 pekee kabla ya kulazimika
kutoka nje baada ya kupata jeraha jengine.
''Kama matokeo yangalikuwa 2-0
asingecheza.Lakini ilibidi tumchezesha .Kitengo
changu cha matibabu kiliamua kumchezesha'',
alisema Mourinho.
Amsema kuwa mshambuliaji huyo atakuwa nje
kwa wiki mbili .
Hii inamaanisha kwamba Costa ataikosa mechi
dhidi ya QPR tarehe 12 mwezi Aprili na ile dhidi
ya Manchester United katika uwanja wa Stamford
Bridge tarehe 18 mwezi Aprili.
Category:
0 comments