.

.

BIASHARA KWA KUTUMIA SIMU YA KIGANJANI

ZePLAN | 16:23:00 | 0 comments

Watu wengi hawajui kuwa kupitia simu
yako ya mkononi, tabiti, au kompyuta
yenye mtandao, unaweza kununua
bidhaa zako na kuzipata kwa muda
mfupi mlangoni kwako.
Kasi ya ukuaji wa Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano (Tehama) imefungua
milango ya kununua bidhaa mtandaoni
kwa kuyavuta maduka na kupunguza
utegemezi wa kununua bidhaa kwa
kuonana na muuzaji.
Kampuni kadhaa za nje na za ndani
kama Kaymu, Hellofood, Kivuko, Jumuia,
ShoppingTz na nyinginezo, zimeanzisha
huduma hiyo ili kutumia fursa adhimu
ya biashara katika jamvi la Tehama.
Biashara hii inafanyikaje?
Katika soko au duka la mtandaoni, mteja
na muuzaji hawakutani ana kwa ana,
bali kupitia mtandao kwa kuunganishwa
kupitia tovuti au programu ya simu
(‘app’) ambazo nyingi humilikiwa na
kampuni za kijasiriamali.
Tovuti hizo huwa ni jamvi au meza
ambazo wauzaji huweka taarifa zao za
kina kama vile bei na aina ya bidhaa,
idadi, kiwango, mwaka wa
kutengenezwa (kwa bidhaa za kuisha
muda) na uwezo wake.
Taarifa hizo huambatana na picha halisi
za bidhaa ili kuzuia utata unaoweza
kutokea mteja anapokuta bidhaa
aliyonunua na kuletewa siyo ile iliyopo
pichani. Programu ya kompyuta
inayofanya kazi kama kikapu hutumika
kufanikisha ununuzi kwa kumjulisha
mnunuzi jumla ya bidhaa alizonunua na
fedha anazodaiwa.
Katika tovuti hizo kuna kila aina ya
bidhaa kuanzia nguo, vyakula, magari,
vitabu, vifaa vya elektroniki, vipodozi,
vidani, muziki, video na vinginevyo.
Malipo
Malipo katika biashara hiyo
iliyoanzishwa miaka 35 iliyopita na
mjasiriamali Mwingereza Michael
Aldrich, yanaweza kufanyika moja kwa
moja mtandaoni au wakati mteja
anapopokea bidhaa.
Meneja Mkuu wa kampuni ya kuuza
chakula mtandaoni, Sherrian Abdul
anasema wateja wanaweza kulipia
kupitia Tigo Pesa (kwa sasa) au kulipia
wakati wanapokea chakula.
Pia, shoponlinetz kupitia tovuti yao
wamebainisha kuwa wateja wanaweza
kufanya malipo yao kupitia kampuni za
malipo za Visa, Visa Electron, Paypal,
Mastercard, Airtel Money na Tigo pesa.

Kwa maoni na ushauri:
Ochec54@gmail.com

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments