IBADA YA KATISHWA KANISANI KWA HOFU YA UGAIDI
Ibada yakatishwa katika kanisa moja la Kianglikana nchini
Kenya ilikatizwa ghafla baada ya tishio la ugaidi
siku ya Jumapili.
Waumini walihamishwa kutoka kanisani hilo
baada ya gari moja kuingia ndani ya uwanja wa
kanisa kimabavu.
Kenya iko katika hali ya tahadhari baada ya
mauaji ya watu wasiopungua 150 kaskazini mwa
taifa taifa hilo.
Ibada hiyo ya Pasaka iligeuka na kuwa mbio za
mguu niponye baada ya waumini kuarifiwa
kuhusu gari hilo lisilo na nia njema.
Askofu wa kanisa hilo, Julius Kalu, amesema
aliarifiwa kuhusu gari ambalo liliingizwa ndani ya
uwanja wa kanisa bila hilo idhini kabla ya
kusimamishwa kwenye lango kuu la kanisa
lenyewe.
Askofu Kalu amesema waliokuwa ndani ya gari
hilo walitoroka
Polisi waliitwa, na baada ya kulikagua gari hilo
walilivuta hadi makao makuu ya polisi.
Mkuu wa polisi eneo la Mombasa Robert Kitur
amesema hawakupata kitu, lakini wamelizuia gari
hilo kwa uchunguzi zaidi.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza
kumshirikisha mwenzako
Category:
0 comments