.

.

Google yaja kivingine yazindua huduma nyingine Marekani

ZePLAN | 20:41:00 | 0 comments

Kampuni ya Google imatangaza kuwa itazindua
huduma mpya nchini Marekani ambayo inaweza
kutumiwa nyumbani na wakati wa safari za
mataifa ya kigeni.
Huduma hiyo inayo fahamika kama Project Fi
inatapatikana kwa simu za Smartphone za
Google Nexus 6.
Huduma hiyo itatumia maeneo yaliyo na Wi-Fi
sambamba na huduma zingine za mawasilianoi
nchini Marekani za Sprint na T-Mobile na
inaweza pia kutumiwa kwenye nchi 120 bila
malipo ya ziada wakati mtu anaposafiri nje ya
nchi.
Huduma hiyo itatolewa kwa malipo ya dola
ishirini kwa mwezi kwa huduma za kawaida na
dola kumi kwa mwezi kwa kila gigabyte ya data
inayotumika.
Google inasema kuwa huduma hiyo huwa
inajiunga moja kwa moja na zaidi maeneo milioni
yenye huduna za Wi-Fi na mteja ana uwezo wa
kuhamiswa kutoka kwa mtandao mmoja hadi
mwingine kulingana na ni upi unaotoa huduma
bora zaidi.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments