.

.

RAISI WA TANZANIA JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA ZOEZI LA USAFI

ZePLAN | 22:00:00 | 0 comments


Magufuli

Picha juu Raisi John Pombe Magufuli katika fukwe akifanya usafi

Raia nchini Tanzania wameungana na maafisa wa serikali kuitikia wito wa Rais John Magufuli wa kutumia Siku ya Uhuru kufanya usafi.
Mamia ya watu walirauka na kuanza kusafisha baadhi ya maeneo ambayo hujulikana sana kwa kuwa na uchafu na taka kwa wingi.
Wachuuzi na maafisa wa baraza la jiji Dar es Salaam asubuhi na mapema wakifanya usafi katika soko maarufu la Kariakoo.

 Usafi
 Picha juu watumishi kataki shughuli ya usafi
Wengi wamefurahia agizo la  Mh Rais.
Hata hivyo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pia amefika soko hilo la Kariakoo.kwa ajili ya kushughulika na zoezi zima la usafi kama agizo la rais linavyosema.
Rais John Magufuli naye amekuwa kwenye aneo la ufuo wa bahari karibu na ikulu akiwa amevalia glavu.
  "HAPA KAZI TUU"

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments