.

.

MAKOSA 10 YA KUEPUKA KWENYE MATUMIZI YA FEDHA

ZePLAN | 08:31:00 | 1 comments

Si jambo la ajabu kumsikia mtu akisema fulani
ana matumizi mabaya ya pesa au yule akipata
pesa zinamtawala.
Hata hivyo, tunashindwa kutambua kuwa hiyo si
njia ya kumsaidia mtu wa aina hiyo kwani
hawezi kubadilika.
Mtu huyo tunamuona mfujaji wa pesa kutokana
na ukweli kuwa hajui jinsi ya kushughulikia tatizo
alilonalo.
Ni vema ukatambua kuwa, kamwe huwezi
kubadilisha mwenendo wako kuhusu hali ya
kifedha, isipokuwa unaweza kushughulikia baadhi
ya matatizo.
Hii inahusu tabia ya kufanya au kutofanya
mambo fulani. Tabia zetu nyingi kuhusu pesa
huundwa bila ya sisi kujitambua au kutojali
katika kipindi kirefu.
Hakuna hata mmoja wetu ambaye hukaa chini
na baada ya kufikiri kwa muda mrefu, akatoka
na jibu kwamba, kuwa na uwiano katika kitabu
cha hundi ni jambo la kijinga. Badala yake tabia
huibuka yenyewe baada ya muda mrefu.
Tabia yetu kuhusu pesa husababishwa na namna
tunavyotunza pesa, tunavyotumia,
tunavyothamini na tunavyofikiri kuhusu
mustakabali wetu. Hivyo kile tutakachojifunza
kuhusu pesa, kinaweza kufanya tuwe na
mwenendo mzuri au mbaya wa pesa zetu.
Ni vema ukakumbuka kuwa, unapogundua juu ya
jambo fulani ambalo limekosa mwenendo mzuri,
basi utafute namna ya kuachana nalo.
Acha kurudia makosa yale yale kila mwaka na
ujiulize ni kwa nini huweki akiba kutokana na
kipato chako? Njia pekee ya kuepekuna na tabia
hiyo ni kufuta mfululizo wa makosa hayo yenye
tabia ya kujirudia na udhamirie kubadili maisha
yako.
Baadhi ya watu huishi huku wakiendelea kurudia
makosa katika sekta ya kiuchumi. Bila shaka
hutakiwi kuwa mmoja wa watu wa aina hiyo.
Ili uepukane na mkosaji anayerudia kosa,
unapaswa kuhakikisha kuwa hufanyi kosa lolote
miongoni mwa makosa haya kumi ambayo wengi
wetu huyafanya kuhusu pesa.
Hata hivyo unapaswa kuhakikisha kuwa
unaitambua vyema hali halisi ya gharama
duniani, huku ukichagua njia muafaka ya
kukabiliana na kila hali.
1. Kutumia pesa bila ya bajeti
Mara nyingi watu hufikiri juu ya mipango
mbalimbali ya kuwaingizia fedha, mfano wapo
wanaofikiri ni jinsi gani watawekeza ili kuifanya
pesa hiyo iongezeke, lakini ni wachache sana
ambao hufikiri juu ya kuandaa bajeti, hasa kwa
kuzingatia uwezo wao kifedha.
Mshauri mmoja wa masuala ya kifedha kutoka
nchini Marekani, John Ritter, aliwahi kusema
iwapo una kipato na Ankara, unahitaji pia kuwa
na bajeti.
“Mara nyingi kuna kikubwa kinachotoka kuliko
kipato,” anasema.
Je, kutumia pesa bila bajeti kunaweza
kukugharimu nini? Wengi wetu wanaweza
wasikubaliane na hili kwa kuamua kutokubaliana
nalo, au wamekuwa wakisumbuka bila ya
kuelewa kinachowasumbua.
Jambo hili si jingine, isipokuwa kukosa utulivu
wa akili na mawazo kuhusu pesa pamoja na
uwezo wa kuandaa bajeti ya muda mrefu.
Mwisho wa hali kama hii ni kushindwa kuwa
sahihi juu ya kile ulichotumia kuwa ni asilimia 15
au 20 au zaidi katika chakula au afya.
Namna ya kuepukana na athari hiyo, hakikisha
unaweka utaratibu wa kutambua kila aina ya
matumizi unayoyafanya ili kung’amua ni wapi
pesa zako zinakwenda.
Njia nzuri ya kumudu jambo hilo ni kuhakikisha
unaorodhesha mahitaji yote ambayo hayalipwi
kwa utaratibu wa ankara, mfano vinywaji,
burudani mbalimbali, kuchangia sherehe
miongoni na mengine mengi.
Baada ya kufanya hivyo hakikisha unatenga kiasi
fulani cha pesa kwa ajili ya dharura, mfano
matengenezo ya gari iwapo umebarikiwa kuwa
nalo, au hata pesa ambayo itakuwezesha kusafiri
kwenda kuona mgonjwa au kuhudhuria msiba.
Watu wengi hudharau mahitaji ya aina hii na
kuyaweka kando ya bajeti kwa sababu hayana
umuhimu kwao.
Hata hivyo, mara yanapotokea, umuhimu wake
huonekana na hapo ndio hutambua kuwa kumbe
katika wakati wote kuna matumizi.
2. Kutembea na kadi inayoruhusu ukope
Hili ni tatizo kubwa kwa nchi za wenzetu
walioendelea, na wengi hifikiri kuwa hiyo ni
sehemu ya ustaarabu na maendeleo.
Kutembea na kadi inayoruhusu ukope, ni hatari
kwani inakufanya kuwa na tamaa ya kupata
mahitaji. Sharti la ukopaji wa aina hii ni kukatwa
riba kubwa ikilinganishwa na mtu anayenunua
moja kwa moja.
Hapa kwetu kuna taasisi na mashirika yanayotoa
huduma na vitu kwa njia ya mkopo, lakini iwapo
utachunguza vema, utagundua kuwa muda
ambao unakaa na deni unakugharimu zaidi,
kwani utalazimika kulipa kwa asilimia kadhaa
zaidi ya yule aliyenunua kwa kulipia moja kwa
moja.
“Mara nyingi watu wanaotaka kulipia huduma au
kitu kidogo kidogo hawawezi kufanya chochote
na badala yake wanapata hasara kubwa,”
anasema John Ritter.
Kwa ujumla kadi za aina hii ni njia mojawapo ya
kukufanya uwe mtumwa wa mahitaji yako au
madeni.
Ushauri ambao ningependa kukupatia hapa ni
kwamba, hakikisha unafanya malipo
yanayotakiwa kwa wakati na usikubali kubaki na
deni lisilo la lazima.
Baada ya hapo, hatua inayofuata ni kuhakikisha
kuwa unadhamiria kwa hali na mali, hata
ikiwezekana kwa kujinyima, ili uweze kulipa na
kuachana na madeni hayo kabisa, ukianza na
moja na baada ya jingine.
Tambua kuwa siku zote deni kubwa ni gumu
kulimaliza, lakini hiyo isikukatishe tamaa na
badala yake ione kuwa changamoto kwako.
Iwapo ulifurahia matunda ya deni hilo, basi uwe
tayari kubeba mzigo wake.
Kwa ujumla njia rahisi ya kuepukana na madeni,
ni kuhakikisha kuwa unalipia mahitaji yako yote
kwa ukamilifu, kila ifikapo mwisho wa mwezi.
Iwapo utahitajika kutumia kadi inayokuruhusu
kukopa wakati una dharura, basi hakikisha kuwa
unakopa kiasi cha kutosha kukidhi dhahruara
hiyo tu (mfano, ugonjwa, ajali au safari).
Baada ya kufanya matumizi hayo, hakikisha
kuwa hutumii kadi hiyo hadi utakapokamilisha
malipo ya deni hilo.
3. Kudharau riba zitolewazo na benki
Bila ya kujali kiwango cha riba kinachotolewa
katika masoko ya hisa, mabenki au kuwekeza
katika taasisi zinazotoa mikopo kwa ajili ya
ujenzi wa nyumba, ni jambo la muhimu kuweka
pesa katika taasisi zinatoa riba.
Unaweza kujenga utaratibu wa kununua hisa
katika makampuni, mashirika au hata taasisi za
fedha. Jambo la kuzingatia, ni kwamba, hii ni
njia ya kuzalisha pesa ambazo huzitumii kwa
sababu siku utakapoamua kuuza hisa hizo au
kuhitaji pesa zako, hazitarejea kama zilivyokuwa,
zitaongezeka.
Ipo faida ya kuwa mwanachama unayechangia
katika taasisi zinazotoa mikopo, kwani hupata
unafuu wakati wa kurejesha mkopo huo.
Mfano, mwanachama anayekopa kutoka taasisi
ambayo hutoa mikopo kwa ajili ya ujenzi wa
nyumba, ni wazi kuwa atapata unafuu wakati wa
kurejesha mkopo huo kuliko mtu anayekopa
wakati si mwanachama, kwani riba ya urejeshaji
wa mkopo wake itakuwa ya juu zaidi.
Kwa leo tuishie hapa, juma lijalo tutaendelea na
makosa yaliyosalia.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

1 comment: