POLISI WASHINDWA KUMHOJI GWAJIMA
Dar es Salaam . Jeshi la Polisi Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam, jana
lilishindwa kuendelea kumhoji Askofu
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat
Gwajima kuhusu tuhuma za kumtukana
Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Askofu Gwajima alifika katika Kituo
Kikuu cha Polisi (Central), jana
asubuhi,ikiwa ni siku mbili tangu
aliporuhusiwa kutoka katika Hospitali ya
TMJ alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Wakili wa askofu huyo, John Mallya
alisema jana kuwa mteja wake alifika
kituoni hapo saa 2.10 asubuhi, lakini
Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi Kanda
ya Dar es Salaam alipomuona, alisema
hawawezi kumhojiano kwa kuwa afya
yake haijaimarika.
“Alitutaka turudi na badala yake kufike
kituoni hapo Aprili 9, mwaka huu,”
alisema Wakili Mallya aliyeongozana na
Askofu Gwajima pamoja na wachungaji
wanane wa kanisa hilo.
Askofu Gwajima alijisalimisha
mwenyewe kituoni hapo Ijumaa
iliyopita, baada ya kutakiwa kufanya
hivyo na Jeshi la Polisi, akituhumiwa
kumkashfu Kardinali Pengo wa Kanisa
Katoliki Jimbo Kuu Dar es Salaam,
wakati akiendesha ibada kanisani
kwake.
Awali, wakati akihojiwa, aliishiwa
nguvu na hatimaye kupoteza fahamu,
hivyo kupelekwa hospitali kwa
matibabu.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya
ya Kinondoni, Paul Makonda amesema
Askofu Gwajima lazima atahojiwa na
ofisi yake ili kujiridhisha zaidi na
shughuli anazozifanya, ikiwamo umiliki
na uhalali wa kutumia eneo la Kiwanja
cha Tanganyika Packers, kilichopo
Kawe.
Makonda aliyezungumza kauli hiyo
akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi
na Usalama wilayani hapo, alisema
lengo la uamuzi huo ni kuepuka athari
zinazoweza kujitokeza.
kwa ushauri na maoni tuandikie: ochec54@gmail.com
Category:
0 comments