TANZANIA:SERENGETI BOYS YATOKA SARE NA TIMU YA VIJANA WA GHANA(BLACK STARLETS)

Katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki Ghana ama black Starlets ndio walianza kuziona nyavu za Serengeti kwa mabao ya Sulley Ibrahimu dakika ya 30 na Arko Mensah dakika ya 73.

Serengeti walisawazisha magoli hayo kupitia kwa Asad Juma kwa penalti na Muhsin Malima mabao yote yakifungwa dakika za nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida za mchezo
Huo ulikuwa mchezo wa tatu wa majaribio katika maandalizi ya Serengeti Boys kujianda na fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, michuano itayofanyika nchini Gabon.
Category:
0 comments