.

.

NEPAL:zaidi ya watu 5000 wapoteza maisha

ZePLAN | 09:38:00 | 0 comments

Majengo yaliyoporomoka Nepal.
Idadi ya watu ambao wamethibitishwa kuaga dunia wakati kulipotokea tetemeko kubwa la ardhi nchini Nepal siku ya Jumamosi imepanda hadi zaidi ya watu 5000.
Utawala unasema kuwa zaidi ya watu 10,000 walijeruhiwa. Serikali ya Nepal inasema kuwa imelemewa na kiwango cha janga hilo.
Waziri mkuu Sushil Koirala anasema kuwa utawala unapokea maombi mengi ya kutaka msaada kutoka maeneo ya mbali ya vijiji vya Himalaya, lakini jitihada za kuyafikia maeneo hayo zinatatizwa na uhaba wa vifaa na waokoaji.
Waziri huyo mkuu anasema kuwa kuna mahitaji ya dharura ya mahema , chakula na maji.zaidi ya nusu ya nyumba katika kijiji hicho zimeharibiwa vibaya na wananchi wake hawana makazi.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments