NOKIA kununua ALCATEL -LUCENT
Chini ya mkataba wa kununua hisa zote,wamiliki
wa hisa za Alcatel-Lucent watamiliki asilimia
33.5 ya kampuni hiyo mpya huku wamiliki wa
hisa za Nokia wakichukua asilimia 66.5.
Kampuni zote mbili zimesema kuwa wakurugenzi
wake wamekubaliana ununuzi wa Alcatel-Lucent
na wanatarajia mpango huo kuafikiwa katika nusu
ya kwanza ya mwaka ujao.
Muungano huo utabuni kifaa cha mawasiliano
barani Ulaya kitakachogharimu yuro billioni 40.
Mkuu wa kampuni ya Nokia Rajeev Suri amesema
kuwa kampuni hiyo ilio na teknologia chungu
nzima itawasaidia kuongeza ujuzi katika kila
sehemu watakayochagua kushindana.
''Ninaamini kwamba huu ni mpango kabambe
uliofanyika wakati mzuri.''
Category:
0 comments