KANYE WEST azindua biblia yake
Hujulikana sana kwa maringo yake,lakini kwa
kweli Kanye West asingekufuru na
kujitambulisha kama mungu katika biblia hiyo.
Kitabu hicho kitukufu kimebadilishwa na kuwa
Biblia ya sasa kwa jina ''Yeezus'' na amini
usiamini kila neno la Mungu katika kitabu hicho
limeondolewa na badala yake msanii huyo wa
muziki wa kufoka foka ameweka jina lake.
Kulingana na gazeti la The Independence nchini
Uingereza,kitabu hicho kinasema kuwa katika
kizazi hiki ,Kanye West ndio mkubwa na vilevile
kiongozi wa kidini
Kitabu hicho kinaongezea kwamba ''katika
utangulizi wetu tunamsherehekea Kanye West na
vile alivyotufanyia katika maisha yetu''
Kanye West na mkewe Kim Kardashian
Ijapokuwa Kanye hajatoa tamko lolote kuhusu
wadhfa huo aliojipatia,amekuwa akijifananisha na
Mungu hapo mbeleni.
''Mungu alinichagua mie,alinitengezea njia.Mimi
ni chombo cha mungu'',alisema mwaka 2009.
''Lakini kinachoniudhi maishani mwangu ni
kwamba sitawahi kujiona nikicheza muziki moja
kwa moja''.,aliongezea.
Wasanii wengine waliofananishwa na Yeezy ni
Marilyn Monroe na Michael Jackson.
Category:
0 comments