.

.

Sepp Blatter azidi kung'aa

ZePLAN | 14:19:00 | 0 comments

Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter
amefananishwa na manabii waliopita, kama vile
rais wa zamani wa Afrika kusini hayati Nelson
Mandela pamoja na Winston Churchill wakati
wanachama kumi wa shirikisho la soka la
Amerika ya kaskazini, America ya kati na
muungano wa visiwa vya Caribbea (Concacaf)
wakimuunga mkono kiongozi huyo katika
uchaguzi wa FIFA hapo May.
Azimio hilo la kumuunga mkono Blatter
limefanywa katika mkutano wa (Concacaf). Rais
wa chama cha soka cha jamhuri ya Dominic
Osiris Guzman, amemfananisha rais huyo wa FIFA
na watu mashuhuri walioweka historia duniani
ikiwemo Moses, Abraham Lincoln na Martin
Luther King.
“Jumuia inatuma ujumbe kuw tunaendelea
kumuunga mkono Blatter” alisema rais wa
Concafaf Jeffrey Webb.Blatter ambaye ni raia wa
Uswiss ni mmoja kati ya wagombea wa nne.
Wengine ni pamoja na mchezaji wa zamani wa
kimataifa wa Ureno Luis Figo, Mholanzi Michael
van Praag, na mwana mfalme Prince Ali Bin Al
Hussein ambaye alikuwa pamoja na Blatter katika
mkutano huo wa Alhamis japokuwa akuhutubia.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments