VITUO VIWILI VYA REDIO VYA FUNGWA NCHINI SOMALI
Mamlaka nchini Somalia imevifunga vituo viwili
vya redio nchini humo baada ya kutangaza
habari za wapiganaji wa Al-shabaab kuhusu
shambulio la chuo kikuu nchini Kenya.
Kituo cha redio cha Sky FM na kile cha Shebelle
vilifungwa huku mtangazaji na mkurugenzi
wakikamatwa.
Vikosi vya usalama nchini Somali vimekuwa
vikiwakamata wanahabari ambao hufanya
mahojiano na wapiganaji wa Al-shabaab ama
kutangaza habari zao.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza
Category:
0 comments