KENYA YAOMBOLEZA
ya yaomboleza
Ikiwa siku ya kwanza ya zile tatu za maombolezi
zilizotangazwa na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
imeanza kufuatia shambulizi la chuo kikuu cha
Garissa,makanisa yote nchini Kenya yatajitolea
kuwaombea waathiriwa wa tukio hilo wakati huu
wa sikukuu ya pasaka.
Shambulizi hilo la siku ya Alhamisi liliwaacha
takriban watu 150 wakiwa wameuawa.
Shirika la msalaba mwekundi nchini Kenya
linasema kuwa hadi sasa maiti 54 zimetambuliwa
katika chumba kimoja cha kuhifadhi maiti kwenye
mji mkuu wa Kenya Nairobi.
Bendera ya kenya
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa
idara za usalama zinahitaji kuongeza jitihada za
kupambana na wanamgambo wa Al shabaab.
Chuo cha kutoa mafunzo ya kiislamu
kinacheshimiwa zaidi nchini Misri, Al-Azhar
kimelaani kile ilichokitaja kuwa shambulizi la
kigaidi dhidi ya wanafunzi wasio na hatia.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza
kumshirikisha mwenzako
Category:
0 comments