.

.

SHAMBULIO LA UGAIDI NCHINI KENYA

ZePLAN | 14:02:00 | 0 comments

Baada ya shambulio la kigidi kutokea nchini Kenya kwenye chuo cha Garissa washutukiwa watano wawekwa chini ya ulinzi mkali na askari wa nchini humo

Serikali ya Kenya inasema kuwa watu watano
wanazuiliwa kufuatia shambulizi lililondeshwa na
kundi la Al shabaab kwenye chuo kikuu cha
Garissa ambapo karibu watu 150 waliuawa.
Baadhi ya washukiwa hao walikamatwa
wakijaribu kutorokea taifa jirani la Somalia,waziri
wa usalama nchini Kenya amesema.
Mwanafunzi wa kike ambaye aliponea shambulizi
hilo ambaye alipatikana amejificha saa 48 baada
ya shambulizi hilo kwa sasa anahudumia na
shirika la msalaba mwekundu.
Takriban watu 148 wengi wao wakiwa wanafunzi
waliuawa wakati wapiganaji walipovamia chuo
kikuu cha Garissa.
Kundi la Alshabaab kufikia sasa limeapa
kutekeleza ,mashambulizi mabaya dhidi ya Kenya.
Maafisa wa Polisi wa Kenya
Kundi hilo linasema kuwa vitendo vyake ni vya
kulipiza kisasi vitendo vinavyofanywa na jeshi la
kenya dhidi ya kundi la Alshabaab nchini Somalia.
Alshabaab pia lililaumiwa na shambulizi la West
Gate mjini Nairobi nchini Kenya mwaka 2013
ambapo watu 67 waliuawa.
Tayari maafisa wa polisi katika taifa jirani la
Uganda wanasema wamepokea habari
zinazosema kwamba shambulizi kama hilo
linapangwa nchini humo.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments