.

.

MWANZA:PROF J AZUA GUMZO MWANZA KWENYE KIKAO CHA CHAMA CHA CHADEMA

ZePLAN | 06:56:00 | 0 comments

Mwanza . Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya, Joseph Haule maarufu kwa jina la Profesa J, mwishoni mwa juma aligeuka kivutio kwenye mkutano wa hadhara wa Chadema uliyofanyika kwenye viwanja vya Mbugani mkoani hapa baada ya kutumia njimbo zake kuwananga CCM.
Msanii huyo ambaye ametangaza nia ya kugombea Ubunge Jimbo la Mikumi mkoani Morogoro, alipewa nafasi ya kuhutubia mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo ambao baadaye walimtaka aimbe nyimbo zake za zamani.
Akihutubia kwenye mkutano huo, Haule alisema kuwa ameamua kugombea ubunge Mikumi, baada ya kuona ujumbe wake kupitia nyimbo zake haufanyiwi kazi na kwamba huu ni wakati wake wa kufikisha ujumbe hadharani kwa vitendo.
“Nimekuwa kwenye game (Muziki) miaka 25, lakini licha ya kuimba nyimbo zinazogusa maisha ya watu na kuona ujumbe wangu haufanyiwi kazi, nimeamua kuwafuata hukohuko Dodoma,” alisema Haule na kuongeza:
“Ninagombea Ubunge kupitia Chadema, kwani ninaamini kuwa hicho ndicho chama pekee kinachoweza kuleta ukombozi. Vijana tusilale wala tusifanye makosa kwenye Uchaguzi Mkuu ujao, lazima tufanye mabadiliko ya kweli.”
Haule alisema amedhamilia kuiondoa CCM katika Jimbo la Mikumbi, katika safari ambayo tayari imeonesha kuzaa matunda baada ya wakazi wa jimbo hilo kumpokei vizuri na kumwaahidi kushirikiana naye katika suala uongozi wake. Nami nimewaahidi kuwa sitawaangusha, alisema.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments