.

.

CHINA:SHERIA KALI YAPITISHWA KUHUSU UGAIDI

ZePLAN | 14:00:00 | 0 comments

China yapitishia sheria kali dhidi ya Ugaidi


Bunge la China limepitisha sheria ya kwanza katika taifa hilo inayolenga kukabiliana na tishio la ugaidi.

Sheria hiyo mpya inazishurutisha makampuni ya teknolojia ya mawasiliano kuipatia serikali taarifa nyeti kuhusiano na Mawasiliano.

Aidha kampuni hizo zitalazimika kutoa anuani za siri za watumiaji wake ikiwemo alama za kuficha mawasiliano.

 
Sheria hiyo itaanza kutumika kuanzia Januari mosi mwakani.
Sheria hiyo itaanza kutumika kuanzia Januari mosi mwakani.

Serikali ya Washington hata hivyo imeonyesha wasiwasi wake juu ya sheria hiyo kuwa huenda ikawa na madhara kwa makampuni ya kibiashara ya kiteknolojia na kudidimiza uhuru wa kujieleza.

Serikali ya Uchina yenyewe imesema sheria hiyo ina ulazima hasa kwa wakati huu ambako matukio ya kigaidi hivi sasa yanazidi kuongezeka na kuhamia kwenye mitandao.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments