.

.

TB JOSHUA AINGIA MATATANI TENA

ZePLAN | 00:41:00 | 0 comments

Ajali ya kanisa
Watu zaidi ya 100, wengi wao kutoka Afrika kusini walikufa wakati jengo la kanisa la Muhubiri TB Joshua lilipoporomoka,

 
Watoto wawili wa Afrika Kusini wanamshitaki muhubiri wa kanisa kubwa na maarufu nchinini Nigeria TB Joshua kwa kifo cha baba yao, wakili wao Bolajii Ayorinde amesema.

Wato hao mmoja mwenye umri wa miaka mitatu na mwingine wa miaka sita wamewasilisha nyaraka za mashtaka katika mahakama ya mji mkuu wa Nigeria, Lagos, wakidai fidia ya zaidi ya dola $521,000; kutoka kanisa la Synagogue Church of All Nations, vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti.

TB Joshua
Muhubiri TB Joshua na kanisa lake wamekuwa wakisisitiza kwamba hawana kosa lolote
 
Baba yao alikua miongoni mwa watu 116 waliokufa wakati jengo la makazi yanayomilikiwa na kanisa hilo lilipoporomoka mjini Lagos mwaka 2014.

Mwaka jana mahakama ya uchunguzi wa vifo iliamuru TB Joshua anapaswa kushtakiwa juu ya kuporomoka kwa jengo, akisema kanisa hilo linahusika kwasababu ya uzembe wa kiuhalifu. Muhubiri TB Joshua na kanisa lake wamekua wakikana kufanya kosa lolote.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments