.

.

MKUTANO WA MSUKOSUKO WA HALI YA KISIASA BURUNDI KUFANYIKA LEO

ZePLAN | 22:17:00 | 0 comments



Mkutano wa ngazi za juu wa kujadili hali nchini Burundi utaanza leo mjini Brussels, Ubelgiji mada kuu ikiwa msukosuko wa kisiasa nchini humo na uhusiano wake na Umoja wa Ulaya.
Mkutano huo, ambao utashirikisha viongozi wa ngazi za juu kutoka mataifa ya Afrika Mashariki, unafanyika kutokana na Umoja wa Ulaya kukusudia kuiwekea vikwazo vya kibiashara Burundi.
Umoja wa mataifa umesema kwamba nchi ya Burundi imeshindwa kuheshimu vipengele muhimu katika mkataba wa ushirikiano na kuvitaja vipengele hivyo kuwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu, kanuni za kidemokrasia na utawala wa sheria na kusema kwamba inaangazia zaidi kuanzisha utaratibu wa kufungua kifungu cha 96 cha mkataba huo wa Cotonou.



Burundi

Kwa kanuni ya ibara ya 96 ya mkataba wa ushirikiano wa Umoja wa Ulaya ni kuijengea uwezo nchi ya Burundi ili ichukue hatua katika muda maalum uliowekwa katika maeneo ambayo demokrasia ina walakini, haki za binadamu zinakiukwa na utawala mbovu wa sheria juu ya msingi wa kanuni zilizowekwa katika mkataba wa makubaliano ya mjini Arusha,kinyume na makubaliano hayo ,hatua za kuwekewa vikwazo zitafuata.
Umoja wa ulaya ni mfadhili mkubwa wa Burundi wakati Ubelgiji imeweka makao yake makuu nchini humo na ni nchi ya kwanza baina ya nchi wahisani kwa koloni lake la zamani.
Serikali ya ya Burundi inaandaa bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2016 na nusu ya bajeti yake inategemea misaada ya kigeni.

Katika tukio la hivi karibuni la kurushiana maneno na ubelgiji na umoja wa ulaya ,chama tawala nchini burundi cha CNDD FDD kimesema kwamba nchi hiyo haitahitaji misaada ya kigeni.Baada ya yote hayo chama hicho kikaongeza kwa kusema kwamba asilimilia themanini ya wafadhili inarudi katika nchi za Magharibi.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments