.

.

OSCAR PISTORIUS KURUDI KORTINI LEO

ZePLAN | 22:29:00 | 0 comments

Mahakama

Picha juu mwanarihadha nguli Oscar Pistorius
 
Bingwa wa Olimpiki wa mbio za walemavu kutoka Afrika Kusini Oscar Pistorius, anatarajiwa kurejea kortini leo kwa kikao cha kuomba apewe dhamana.
Hii ni baada yake kupatikana na hatia ya mauaji ya mpenzi wake, kufuatia rufaa ya upande wa mashtaka.
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 28, kwa sasa anatumikia kifungo cha nyumbani kutokana na hukumu ya awali ya kuua bila kukusudia.
Sasa anakabiliwa na uwezekano wa kurejea gerezani ambako atapewa hukumu mpya.
Alikiri kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp, Februari 2013 lakini akasema alidhani ni mwizi aliyekuwa ameingia nyumbani kwake.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments