.

.

MAHAKIMU 20 WAFUTWA KAZI KUOKANA NA RUSHWA

ZePLAN | 22:12:00 | 0 comments

Anas

Mamlaka ya mahakama nchini Ghana imewafuta kazi mahakimu 20 ambao wamehusishwa na sakata la kupokea rushwa.
Miongoni mwa waliotimuliwa ni mahakimu wa mahakama za chini.
Bado kuna baadhi ya mahakimu wa mahakama kuu ambao wamesimamishwa kazi huku uchunguzi zaidi ukiendelea.
Ufisadi huo ulibainika baada ya mwandishi wa habari za uchunguzi, Aremeyaw Anas, alipokusanya kwa muda wa miaka miwili kanda za video za masaa yapatayo 500 kama ushahidi dhidi ya zaidi ya mahakimu 30 na takriban watumizi wa mahakama wapatao mia mbili.
Kutokana na sakata hilo, baadhi nchini Ghana wanataka kuwepo kwa mabadiliko katika mahakama nchini humo.


Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments