MUAFAKA WA AMANI LIBYA WAFIKIA TAMATI
Picha juu wajumbe wakikumbatiana kwa furaha mara tuu baada ya kikao |
Wawakilishi kutoka
mabunge hasimu nchini Libya wametia saini mkataba wa kuundwa kwa
serikali ya umoja, kufuatia mashauriano nchini Morocco.
“Mchakato huu wa mazungumzo umeonyesha kwamba Walibya wanaweza kutatua tofauti zao za kisiasa kupitia mazungumzo ya Amani,” amesema.
Hata hivyo ametaja changamoto nne ambazo serikali mpya inafaa kushughulikia, ambazo ni: mgogoro wa kibinadamu, mashauriano ya usalama wa kitaifa, kukabiliana na kundi la Islamic State na makundi mengine ya kigaidi na kuangazia Benghazi na maeneo mengine.
Akiandika kwenye Twitter, balozi wa Uingereza nchini Libya amesema mkataba huo umepokelewa kwa shangwe na Walibya mjini Skhirat.
Aliekuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi |
Libya ilitumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Category:
0 comments