MWANAANGA AKOSEA NAMBA AKIWA ANGANI NA KUMPIGIA MTU MWINGINE
Picha juu mwanaanga wa kwanza wa Uingereza kwenda kituo cha ISS |
Mwanaanga Tim Peake, ambaye ndiye
Mwingereza wa kwanza kwenda kituo cha kimataifa cha anga za juu, ameomba
msamaha baada ya kupiga nambari ya simu isiyo sahihi kutoka anga za
juu.
Bw Peake amesema kwenye Twitter kwamba simu hiyo haikuwa ya mzaha.
Hata hivyo, hakusema ni nani hasa aliyekuwa akimpigia simu.
Peake, baba wa watoto wawili anayetoka Chichester, Sussex Magharibi, alitua katika kituo cha kimataifa cha anga za juu (ISS) Jumanne 15 Desemba.
Atakaa katika kituo hicho miezi sita akifanya utafiti wa kisayansi.
Mapema wiki hii, aliwasaidia wanaanga wenzake wawili kutoka nje ya kituo hicho.
Wanaanga Tim Kopra na Scott Kelly, kutoka kituo cha Nasa cha Marekani walihitaji kutoka nje ya kituo hicho kukarabati kifaa kilichokuwa kimeharibika.
Category:
0 comments