JESHI LA MAREKANI LAFUKUZWA NA WAASI LIBYA
Wanajeshi wa Marekani waliofika
nchini Libya wamelazimika kuondoka punde baada ya kutua, kutokana na
masharti makali ya kundi la wapiganaji waliodhibiti eneo walilotua.
Msemaji wa idara ya jeshi la Marekani Barani Afrika{Africom} amesema kuwa wanajeshi hao waliamua kuondoka ili kuzuia vurugu.
Libya imekua kwenye machafuko tangu mwaka 2011 baada ya Kanali Muammar Gaddafi, kuondolewa madarakani.
''Wanajeshi hao wa Marekani walikwenda Libya kuimarisha uhusiano na jeshi la taifa'', ameongeza msemaji wa Africom Anthony Falvo.
Mwandishi wa BBC kaskazini mwa Afrika anasema kisa hiki ni aibu kubwa kwa Marekani ambayo ina maslahi mengi ndani ya
Libya, hususan operesheni dhidi ya wapiganaji wa 'Islamic State'.
Libya ina serikali mbili; moja ina makao yake katika mji mkuu Tripoli na nyingine katika mji wa Tobrouk.
Wiki hii pande mbili zilisaini makubaliano nchini Morocco ya kuunda serikali ya muungano wa kitaifa.
Category:
0 comments