.

.

TAKRIBANI WAHAMIAJI MIL1 WAHAMIA ULAYA

ZePLAN | 11:51:00 | 0 comments


Idadi ya wahamiaji na wakimbizi waliongia bara Ulaya kwa kutumia njia za nchi kavu na bahari mwaka huu, imepita milioni moja.

Takwimu za hivi karibuni, zimeonyesha kuwa idadi ya wakimbizi na wahamiaji imeongezeka mara nne ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Shirika la umoja wa matafa linaloshughulikia wakimbizi na lile linaloshughulikia wahamiaji IOM ndiyo yametoa takwimu na taarifa hiyo.

Wengi wao wakitumia njia hatari za kuvuka bahari ya Mediterranean wakitumia viboti vidogo ambavyo havina ubora wa kutumika katika safari za aina hiyo.

Nusu ya wakimbizi hao wanatoroka vita nchi mwao SYRIA.

Mashirika ya kutoa misaada ya huduma za kibinadamu wanatoa wito wakimbizi hao wasaidiwe ili wapitie njia salama wanapotoroka vita na maafa mengineyo na pia wasaidie kupewa makaazi.

 
Takwimu hizo zinaiweka 2015 kuwa mwaka mgumu zaidi kwa wakimbizi tangu vita vikuu vya pili vya dunia.

Ulaya ambao kwa upande wengine wanalaumiwa kuchochea mizozo ya kivita huko mashariki ya kati hasa katika nchi za Libya na Iraq zimehimizwa kusaidaia zaidi kutatua tatizo hilo la wakimbizi.

Zaidi ya wakimbizi 3,600 wamekufa maji katika bahari ya Mediterrania mwaka huu pekee baada ya kukosa usaidizi na kuingia katika safari hizo za hatari zinazopangwa na walanguzi wanaowatoza fedha nyingi.

Wanaofaulu kuvuka salama hukabiliwa na matatizo ya makaazi huku wengi wa wanawake na watoto wakiwa katika hali mbaya zaidi iwe ya kimazingira ,kisaikolojia na hasa upungufu wa chakula .

 
Takriban wakimbizi na wahamiaji 3,700 wameaga dunia wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania.
Hata hivyo mataifa ya muungano ya Ulaya licha ya kufanya vikao vingi kujadili swala hilo bado yamegawanyika sana kuhusu vipi kukabiliana na tatizo hilo.

Ujerumani ndiyo angalau imewapa imewasajili wakimbizi laki 9, wengi ambao walifika ulaya zaidi ya mwaka mmoja uliopita lakini wapo maelfu wengine waliowamba katika mataifa kama Ugiriki ambako wameifanya kama njia tu ya kupitia ili kufika kule wanakohisi watapata usaidizi.

Wachanganuzi wa maswala ya kimataifa wanakubaliana kwamba tatizo hili la mkurupuko wa wakimbizi kukimbilia Ulaya litaendelea hadi pale suluhu ya kudumu lipatikane ya kumaliza vita vya Syria, Iraq.

Takriban wakimbizi na wahamiaji 3,700 wameaga dunia wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments