IRAQ:VIKOSI VYA SERIKALI VIKISHIRIKIANA NA VIKOSI VYA KIKABILA KUPAMBANA VYAKOMBOA MJI WA RAMADI
Mamlaka nchini Iraq inasema kuwa
vikosi vya serikali vimeanzisha mashambulizi makali ya kukomboa eneo la
katikati mwa mji wa Ramadi, ambalo limekuwa chini ya udhibiti wa
wapiganaji wa Islamic State tangu mwezi wa Mei.
Serikali ya Iraq imefanya ukombozi wa mji wa Ramadi kuwa lengo kuu.
Imekuwa ikijitayarisha kwa miezi kadha, kukata njia za usambazaji wa bidhaa, na mara kwa mara, kuwataka wenyeji mjini humo kuhama.
Swala hilo limekuwa kikwazo kikuu, kwani watu wengi wamesalia mjini humo, na kutatiza mashambulizi ya angani yanayotekelezwa na vikosi vya muungano .
Inakadiriwa kuwa mamia ya wapiganaji wa Islamic State wamesalia Ramadi.
Ripoti kutoka huko zinasema wamekuwa wakijaribu kutuliza uasi dhidi yao, na pia kuwazuia raia kuondoka.
Mamalaka nchini Iraq inasema kuwa vikosi vya kikabila vimejiunga na mashambulizi ya kukomboa mji huo, na kusema kuwa huenda wakaukomboa mji huo ifikapo mwishoni mwa wiki hii.
Category:
0 comments