RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AIGWA NA KIONGOZI WA UPINZANI WA MYANMAR
Kiongozi wa upinzani wa Myanmar, Aung San Suu Kyi
|
Kiongozi wa upinzani wa Myanmar, Aung San Suu Kyi, leo alivaa glavu na kuokota taka katika tarafa yake.
Majuzi
bi Suu Kyi, aliwaomba wabunge wa chama chake waliochaguliwa hivi
karibuni, kwamba waokote takataka, kama sehemu ya kampeni ya kufanya
usafi nchini.Chama chake cha NLD kilishinda viti vingi katika uchaguzi uliofanywa mwezi uliopita.
Serikali ya sasa ya kijeshi, imeteua kamati kusimamia shughuli ya kukabidhi madaraka chama cha bi Suu Kyi.
Uchafu ni tatizo la taifa nchini Myanmar, ambayo haina mfumo hasa wa kukusanya taka na kuzitupa.
Picha juu Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli katika ubora wake |
Rais wa Tanzania Joseph Pombe Magufuli, aligonga vichwa vya habari kote duniani alipochukua jukumu la kusafisha mji mkuu wa Dar es Salaam Tanzania badala ya kuongoza sherehe za kuadhimisha sikuu ya kitaifa.
Category:
0 comments