JOHNSON & JOHNSON KULIPA FIDIA YA $72 M
Poda ya Johnson inasemekana kuwa chanzo cha saratani ya ovari iliyomuua Jackie Fox |
Jopo la mahakama katika jimbo la
Missouri limeiamrisha kampuni ya Johnson & Johnson (J&J) kulipa
dola milioni 72 kwa familia ya mwanamke aliedai kifo chake kilikua na
uhusiano na matumizi ya poda ya watoto ya talc, inayotengenezwa na
kampuni ya Johnson&Johnson.
Familia ya Jacky Fox inasema alipata satarani ya Ovari baada ya kutumia poda ya Johnson&Johnson |
"tunaionea huruma familia ya mlalamikaji , lakini tunaamini kabisa usalama wa kipodozi talc umekua ukifuatiliwa kwa miongo kadhaa na ushahidi wa kisayansi upo."
Uamuzi huo uliotolewa baada ya kesi iliyochukua wiki tatu ni wa kwanza ambapo jopo la Mahakama ya Marekani limeamuru kulipwa kwa gharama kwa madai kuhusiana na poda ya talc. Zaidi ya visa 1000 vya aina hiyo viko kote nchini Marekani na mawakili wanasema maelfu zaidi ya watu wanaweza kuwasilisha kesi zao Mahakamani.
Category:
0 comments