BARCELONA NA BAYERN MUNICH ZATINGA ROBO FAINALI (UEFA)
Ligi
ya Mabingwa Ulaya iliendelea jana usiku kwa michezo miwili ambapo
Barcelona ilikuwa mwenyeji wa Arsenal katika uwanja wa Nou Camp na
Barcelona ikiibuka na ushindi wa goli 3 – 1.
Magoli
ya Barcelona yalifungwa na Neymar dk. 18, Luis Suarez dk. 65 na Lionel
Messi dk. 79 huku goli pekee la Arsenall likifungwa na Mohamed Elneny
katika dakika ya 51 na hivyo ushindi huo kuiwezesha Barcelona kufuzu kwa
magoli 5 – 1.
Mchezo
mwingine ulikuwa ni Bayern Munich iliyokuwa mwenyeji wa Juventus katika
uwanja wa Allienz Arena na Bayern kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli
4 – 2.
Juventus
ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata kupitia kwa Paul Pogba dk. 5 na baadae
dakika ya 28 ikapata goli la pili kupitia Juan Cuadrado magoli
yaliyodumu hadi pumziko.
Kipindi
ca pil Bayern ilisawazisha kupitia Roberto Lewandowski dk. 73 na Thomas
Muller dk. 90 na hivyo kumaliza mchezo wakiwa sare ya goli 2 – 2.
Bayern
ikaongeza magoli mengine mawili katika dakika 30 za nyongeza kupitia
Thiago Alcantara dk. 108 na Kingsley Coman dk. 112, na hivyo kuibuka na
ushindi wa goli 6 – 4.
Unaweza kutizama vdeo za magoli hapa chini............
Category:
0 comments