.

.

CHELSEA YAKUBALI KICHAPO CHA 2-1 KUTOKA KWA PSG

ZePLAN | 00:21:00 | 0 comments

chelsea vs psg
Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, iliyochezwa usiku wa jana Jumatano kwenye viwanja viwili tofauti,  ikiwemo uwanja wa Stamford Bridge uliyopo jijini London na Petrovsky uliopo nchini Urusi .

Jiji la London,wenyeji Chelsea wamelazimika kuchezea kichapo cha pili mfululizo toka kwa PSG kutoka jijini Paris nchini Ufaransa kwa kufungwa bao 2-1, ambapo ushindi huo ni kama ule walioupata timu hiyo ya PSG katika mchezo wao wa awali na kwa maana hiyo, PSG wameweza kujipatia pointi 6 muhimu na magoli 4, huku Chelsea wao wakiambulia mabao yao 2.

Kwa hatua hiyo, PSG  anaingia hatua ya robo fainali katika michuano hiyo mikubwa kabisa barani Ulaya..PSG ilikuwa inahitaji ushindi wa aina yoyote ili kuweza kusonga mbele au sare, hivyo kwa ushindi huo imefuzu hatua ya robo fainali.

Mchezo mwingine umechezwa nchini Urusi , wenyeji Zenit wameweza kulala kwa bao 2-1 dhidi ya Benfica ya nchini Ureno.

Katika mchezo wa awali Benfica walikuwa nyumbani na walifanikiwa kushinda bao 1-0, kwa hatua hiyo Benfica wamefanikiwa kuingia hatua ya robo  ya michuano hiyo kwa jumla ya poiti 6 huku ikijipatia mabao 3, dhidi ya moja la wapinzani wao hao.

abrMchezaji wa PSG, Ibrahimovic akipachika bao  wavuni..dhidi ya Chelsea usiku huu na kufanya matokeo 2-1.
bMchezaji wa PSG, Ibrahimovic akishangilia bao lake aliloifungia PSG  dhidi ya Chelsea usiku huu na kufanya matokeo 2-1.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments