Staa wa muziki nchini, Diamond Platinumz hivi karibuni amepata nafasi ya kuzungumza na Rais Dk. John Pombe Magufuli ambapo alizungumza nae mambo mbalimbali kuhusiana na sanaa ya Tanzania.

Akizungumza na Clouds Fm kupitia kipindi cha XXL, Diamond amesema alizungumza na Rais Magufuli na kumwomba kuwaangalia na wasanii angala kujenga ukumbi mmoja mkubwa ambao utaingiza hata watu 30,000.

Amesema limekuwa jambo la kawaida wanapoenda nchi zingine kunakuwepo na kumbi kubwa lakini kwa hapa nchini ambapo muziki unaonekana kukua kwa kasi kunakosekana ukumbi hata mmoja ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua watu wengi.

“Nimemwambia mheshimiwa atusaidie hata ukumbi mmoja ambao unauwezo wa kuingiza hata watu 30,000 … kuna kipindi nimewahi kuzungumza na Trace na MTV wakataka kuleta tuzo hapa lakini hakuna ukumbi ambao tunaweza kutumia,” alisema Diamond.

Aliongeza kuwa baada ya kumwambia hivyo, Rais Magufuli alimwambia kuwa atalishughulikia jambo hilo kwahiyo wanasubiri kuona hatua gani itafuata.