MRATIBU MKAZI WA UN ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHAKATA MUHOGO RUFIJI
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez amefanya ziara ya kutembelea
mradi wa kiwanda cha kuchakata zao la muhogo ‘African Starch Project’
kilichopo Kata ya Bungu, Wilaya ya Rufiji Mkowa wa Pwani kuangalia namna
kiwanda hicho kinavyo ongeza thamani za zao la muhongo na kuboresha
kipata cha wakulima.
Katika
ziara hiyo, Bw. Alvaro Rodriguez aliongozana na Kiongozi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika ambaye
shirika lake limekubali kusaidia kukiendeleza kiwanda hicho kupata
mashine ya kisasa pamoja na uwezo wa nguvu kazi kuongeza ufanisi wa
kiwanda.
Akizungumza
katika kiwanda hicho, Bw. Malika alisema UNCDF imekubali kukisaidia
kiwanda hicho ili kuinua hali ya kipato cha wakulima wa zao la muhogo wa
Wilaya ya Rufiji ambao tayari walianza kuzalisha mazao hayo kwa
kukitegemea kiwanda cha ‘African Starch Project’ ambacho kilisimamisha
uzalishaji kutokana na uwezo mdogo wa mashine zake.
“…UNCDF tumekubali
kutoa mtaji wa kuanzia pamoja na kuwezesha nguvu kazi ili kiwanda kiweze
kujiendesha kibiashara na kuendelea kuwanufaisha wakulima wa zao la
muhogo eneo hili…tayari wamehamasika na kilimo hiki baada ya kuletwa kwa
mradi huu sasa tunataka kuuongezea nguvu zaidi,” alisema Kiongozi na
Mshauri wa Ufundi wa Shirika la UNCDF, Malika.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) pamoja na Kiongozi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika
(kushoto) wakiangalia sehemu ya tawi la mmea wa muhogo uliopo shambani
walipotembelea moja ya mashamba ya wakulima wa mihogo Wilaya ya Rufiji
jana.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch
Development, Ibrahim M. Hape waendeshaji wa mradi huo alisema kwa sasa
wakulima zaidi ya 500 wa zao la muhogo wameanza kunufaika na mradi huo
ambao wamekuwa wakitegemea kukiuzia kiwanda muhogo wa kuchakata jambo
ambalo limekuza kipato chao.
Alisema
ufadhili wa UNCDF utakapokamilika kimtaji katika kiwanda chao zaidi ya
wakulima 7000 watakuwa wakinufaika ndani ya miaka miwili, ambapo zao
wanalolilima litaitajika kwa wingi kiwandani hivyo kuboresha hali za
kiuchumi kwa jamii, lakini lengo kwa hapo baadaye ni kuhakikisha
wakulima 10000 wananufaika na shughuli nzima za mradi huo wa kiwanda.
Aliongeza
kuwa kwa sasa zaidi ya vijiji 20 wilayani Rufiji vinavyozunguka kiwanda
hiko wananchi wake wapo tayari kufanya biashara ya kilimo kukipatia
kiwanda muhogo wa kuchakata, ambapo watakuwa wakishiriki kuwawezesha
wananchi katika vikundi ili waweze kufanya uzalishaji wa kutosha
kiwandani.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez(kushoto) akisaini kitabu cha
wageni katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Rufiji walipotembelea ofisi hizo jana. Kulia ni Kiongozi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika.
Kwa
upande wao baadhi ya wakulima wakiwemo akinamama waliozungumza katika
ziara hiyo wamelishukuru shirika la UNCDF kwa kufadhili kiwanda hicho
kwani tendo hilo limewahakikishia upatikanaji wa soko la uhakika kwa zao
la muhogo, ambalo hapo awali lilikuwa likilegalega kutokana na kupoteza
kiasi kikubwa cha mabaki ya zao hilo.
UNCDF
inategemea kutumia takribani shilingi milioni 400 kwa ajili ya
kukiwezesha kiwanda cha kuchakata zao la muhogo ‘African Starch Project’
kilichopo eneo hilo.
Ziara
ya viongozi hao ambao waliambatana na wajumbe wa manamawasiliano wa
mashirika ya umoja wa mataifa iliwafikisha katika Halmashauri ya Wilaya
ya Rufiji na kufanya mazungumzo na viongozi wa halmashauri kujua
changamoto anuai za kijamii.
Mtaalamu
wa Mawasiliano, Ushirikiano na Utafutaji Mitaji kutoka Shirika la Umoja
wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Jacqueline Namfua
akiwatambulisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
(kushoto) na Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya
Mitaji (UNCDF), Peter Malika (katikati) kwenye ofisi ya Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji walipotembelea ofisi hizo
jana.
Ujumbe
huo wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini Tanzania ukiongozwa na
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ukitembelea maeneo
mbalimbali ya kiwanda.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akipata maelezo eneo
ambalo mtambo unaosha muhogo kabla ya kuanza uchakataji. Katikati ni
Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim
Hape akitoa maelezo.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) akipata maelezo
eneo ambalo mtambo unaosha muhogo kabla ya kuanza uchakataji. Katikati
ni Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim
Hape akitoa maelezo.
Ujumbe
huo wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini Tanzania ukiongozwa
naMratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez ukitembelea
maeneo mbalimbali ya kiwanda.
Mkurugenzi
Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim Hape
(kushoto) akielezea namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi. Kutoka kulia
wanaomsikiliza ni Ofisa Habari wa Shirika la Kazi Duniani nchini
Tanzania, Magnus Minja, Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika na Mratibu Mkazi wa Mashirika
ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini,
Bw. Alvaro Rodriguez.
Ujumbe
huo ukipata maelezo sehemu ya mitambo ya kiwanda cha kuchakata zao la
muhogo inavyofanya kazi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS
African Starch Development, Ibrahim Hape (aliyenyoosha mkono).
Mkurugenzi
Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim M. Hape (wa
kwanza kushoto) akiwaelezea wajumbe waliotembelea kiwanda hicho namna
kinavyofanya kazi. Ujumbe huo wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN
nchini Tanzania uliongozwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro
Rodriguez (wa tatu kulia). Kutoka kulia ni Ofisa Habari wa Shirika la
Kazi Duniani nchini Tanzania, Magnus Minja na Peter Malika Kiongozi wa
UNCDF.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) akizungumza na
baadhi ya wakulima wanaonufaika na kiwanda cha kuchakata zao la muhogo
‘African Starch Project’ kilichopo Kata ya Bungu, Wilaya ya Rufiji Mkowa
wa Pwani jana walipofanya ziara katika mradi huo uliombioni kusaidiwa
na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) kwa
manufaa ya wakulima wa muhogo eneo hilo.
Mmoja
wa wakulima wa muhogo wanaonufaika na uwepo wa kiwanda cha kuchakata
zao la muhogo ‘African Starch Project’ kilichopo Kata ya Bungu akielezea
wanavyonufaika kwa ujumbe wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini
Tanzania walipotembelea mradi huo jana Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akizungumza na
baadhi ya wakulima wanaonufaika na kiwanda cha kuchakata zao la muhogo
‘African Starch Project’ kilichopo Kata ya Bungu, Wilaya ya Rufiji Mkowa
wa Pwani jana walipofanya ziara katika mradi huo uliombioni kusaidiwa
na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) kwa
manufaa ya wakulima wa muhogo eneo hilo.
Kiongozi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter
Malika akizungumza na baadhi ya wanahabari na ujumbe wa wanamawasiliano
(hawapo pichani) baada ya ziara ya kukitembelea kiwanda cha kuchakata
zao la muhogo ‘African Starch Project’ kilichopo eneo la Bungu Wilaya ya
Rufiji jana.
Mmoja
wa wakulima wa muhogo wanaonufaika na uwepo wa kiwanda cha kuchakata
zao la muhogo ‘African Starch Project’ kilichopo Kata ya Bungu akielezea
wanavyonufaika kwa ujumbe wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini
Tanzania walipotembelea mradi huo jana Wilaya ya Rufiji Mkowa wa Pwani.
Kutoka
kushoto ni Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania,
Hoyce Temu, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
pamoja na Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji
(UNCDF), Peter Malika wakitembelea moja ya mashamba ya zao la muhogo
wilayani Rufiji jana.
Category:
0 comments