JE KUNA UHUSIANO WA KARIBU KATI YA DIAMOND NA OMMY DIMPOZ KWA SASA OMMY DIMPOZ AELEZA
Ommy Dimpoz aliwahi kuwa rafiki mkubwa wa Diamond lakini urafiki wao kwa sasa umeonekana kupungua au haupo kabisa.
Hitmaker huyo wa ‘Achia Body’ ametueleza hali ilivyo sasa.
Amesema hana ukaribu sana na Diamond kwa sasa lakini hana tatizo naye.
“Hapa
hakuna mambo ya kufichaficha, kwamba haina noma hata jana nilikuwa
naye. Vitu viko wazi vinaonekana hatuko karibu kama zamani, hilo liko
wazi. Lakini itakapotokea huko mbele mimi sina tatizo kabisa,” amesema.
Kwa upande mwingine Ommy amedai kuwa anachofanya kwa sasa ni kujikita kwenye mambo yake zaidi.
Category:
0 comments