Kundi la Wasafi Classic (WCB) lililo chini ya NYOTA DIAMOND PLATINUM linataraji kumtambulisha msanii mpya katika kundi hilo Jumatano ya wiki hii Machi, 16.

Taarifa ya utambulisho huo ilitolewa na Diamond kupitia akaunti yake ya Twitter ambapo aliandika “Panapo Majaaliwa Jumatano Hii Wcb_Wasafi tutamtambulisha rasmi Kijana Mwingine Mpya…tafadhali wadau tunaomba sana Support zenu…” ameandika katika ukurasa wake wa twitter