.

.

DONALD TRUMP ASAMBARATISHA CHAMA CHAKE CHA REPUBLICAN

ZePLAN | 23:43:00 |

Christie
Huku ikionekana wazi kuwa kinyang'anyiro cha kiti cha urais wa Marekni kitakuwa ni kati ya Bi Hillary Clinton akipeperusha pendera ya chama cha Democratic na tajiri Donald Trump wa chama cha Republican , wazee na vigogo ndani ya chama cha Reublican hawako radhi kumruhusu tajiri Trump agombee urais.

Wakuu hao wa chama cha Republican wanasema ikiwa watamruhusu Donald Trump awe mgombea urais wao basi kuna uwezekano mkubwa wa chama chao kusambaratika.

Mmoja ya vigogo hao wa Republican, Seneta Lindsey Graham wa South Carolina anasema njia ya pekee ya kumzima tajiri huyo , Donald Trump ni wanachama kumuunga mkono mgombea mwengine wa Republican Bw Ted Cruz.

Aliyekuwa mgombea urais wa chama katika uchaguzi wa miaka mmine iliyopita Bw Mitt Romney pia anasema Bw Trump hafai kuwa mgombea wao japo hadi sasa ameshinda katika majimbo mengi katika kura ya mchujo.

Sasa kibarua kigumu mbele ya wakuu wa Republican ni vipi watamuondoa Bw Trump bila ya kuwakasirisha wafuasi wake ambao wengine ni wa chama cha Demokratic.

Cruz
Ted Cruz ndiye anayeonekana kama anaweza kukabiliana vyema na Trump chama cha Republican
Wachanganuzi wa masuala ya kisiasa wanasema ikiwa Donald trump atanyimwa tiketi ya chama cha Republican basi wanamuona akiamua kugombea urais kama mgombea huru, asiyekuwa na chama.
Hii inatokana na utafiti wa hivi punde unaonyesha kuwa ikiwa Hillary Clinton wa Democratic atasimama na Donald Trump basi utakuwa ni mpambano mkali, hivyo kumjua nani kati yao atashinda urais itakuwa vigumu.

David Merritt wa shirika moja la kutafiti na kutoa ushauri kwa wagombea urais anasema mtu anayemuweza Hilary Clinton ni Bw Trump na anayemuweza tajiri huyo ni Bi Hillary Clinton.

Lakini kadiri siku zinavyo songa mbele hatima ya Donald Trump ndani ya Chama cha Republican itajulikana, kwani tayari mgombea mmoja wa chama cha Republican Ben Carson amesema atajiondoa katika mchuano huo akisema anaweka maslahi ya Wamarekani mbele kuliko yake binafsi.

Kilicho wazi ni kuwa Trump anajua wakuu wa chama cha Republican hawamtaki.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!