JAPAN WAADHIMISHA MIAKA MITANO YA TSUNAMI
Taifa la Japan linaadhimisha miaka
mitano tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi na Tsunami iliosababisha vifo
vya watu 18,000 wengine wakiwa hawajulikani waliko.
Waziri mkuu
Shinzo Abe na mfalme Akihito wanahudhuria makumbusho ya janga hilo mjini
Tokyo na walinyamaza kwa mda ili kutoa heshima kwa wale walioathiriwa.Ukubwa wa tetemeko hilo la 9.0 katika vipimo vya richa lilipiga ufukwe wa bahari wa taifa hilo na kusababisha maji kujaa hatua iliosababisha uharibifu mkubwa kaskazini mashariki mwa pwani ya taifa hilo.
Pia mafuriko hayo yalisababisha janga baya la kinyuklia katika kinu cha fukushima Daiichi .Maji yaliingia katika kinu hicho na kuathiri mashine za baridi hatua iliosababisha mmomonyoko.
Category:
0 comments