Startimes 05 
Kampuni ya ving’amuzi  ya Startimes imekabidhi I Pad 180 kwa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ili kurahisisha utendaji kazi wa Maafisa Habari wa wizara hiyo.

I Pad hizo zimekabidhiwa leo Jijini Dar es salaam na Mtendaji Mkuu wa Startimes  Bw.Lanfang Liao  ambaye amehaidi kutoa misaada ya vitendea kazi  zaidi kwa wizara ili kuongeza ufanisi katika sekta ya habari.

“Kampuni yetu na Wizara ya habari zina ushirikiano wa muda mrefu hivyo, tumeamua kuwakabidhi ipadi 180 zenye thamani ya shilingi milioni 90 ili ziweze kusaidia Wizara katika kazi zake,” alisema Liao.
Bw. Liao ameongeza kuwa, wataendelea kuongeza  chaneli nyingi za Kiswahili zitakazokuwa na maudhui yatakayojikita katika nyanja za utamaduni na Sanaa za kitanzania.

Naye Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye mbali na kuishukuru kampuni hiyo amesema kuwa Ipadi  zitagaiwa  kwa mikoa 15  ambayo maafisa wake wana uhitaji mkubwa wa vifaa hivyo.

“Ni faraja kwamba wenzetu wa Startimes wametuelewa haraka na kukubali kutusaidia vifaa hivi vya mawasiliano (Ipadi) ,kwa hakika vitatusaidia sana kuboresha utendaji kwa maafisa wetu wa Wizara pia Maafisa Mawasiliano ambao ni wadau wa kutoa taarifa kwa Umma,” alisema Nnauye.

Mhe.Nnauye ameongeza kuwa,Wizara ya habari ina lengo la kuimarisha mawasiliano Serikalini kwa kuhakikisha maafisa habari ambao wanafanya kazi kwenye Halmashauri zote kupata vitendea kazi kwahiyo anatoa wito kwa wadau wengine kuendelea kushirikiana na Serikali ili kuboresha mawasiliano kwa Sekta ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.

Hivyo basi maafisa habari wanapaswa kuzitumia Ipadi hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta maendeleo katika sekta ya habari nchini.

Na Shamimu Nyaki – Wizara ya Habari
Startimes 01
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Nape Nnauye ( katika) akisalimiana na Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu You Qing wakati alipowasili katika ofisi za Kampuni ya ving’amuzi ya StarTimes kwa ajili ya kupokea msaada wa iPad kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Maafisa Mawasiliano Serikalini, kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang.

startimes 02
Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu You Qing (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Nape Nnauye kabla ya sherehe za makabidhiano ya  msaada wa iPad kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Maafisa Mawasiliano Serikalini toka Kampuni ya ving’amuzi ya StarTimes, mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Startimes 03
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiteta jambo na Kaimu Mkurugezi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa wakati wa sherehe za makabidhiano ya  msaada wa iPad kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Maafisa Mawasiliano Serikalini toka Kampuni ya ving’amuzi ya StarTimes, mapema hii leo jijini Dar es Salaam (katikati) ni Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rioba.
startimes 04
Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang (katikati) akimtambulisha Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rioba kwa (kushoto) kwa Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu You Qing wakati wa sherehe za makabidhiano ya  msaada wa iPad kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Maafisa Mawasiliano Serikalini toka Kampuni ya ving’amuzi ya StarTimes, mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Startimes 05
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Nape Nnauye ( wa tatu toka kulia) akipokea msaada wa iPad toka kwa Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu You Qing, msaada huo umetolewa na  Kampuni ya ving’amuzi ya StarTimes kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa Maafisa Mawasiliano Serikalini, mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Startimes 06
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rioba akitoa neno la shukrani kwa wageni waliohudhuria sherehe za makabidhiano ya msaada wa iPad 180 kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wenye lengo la  kuboresha utendaji kazi wa Maafisa Mawasiliano Serikalini, mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Startimes 07
Startimes 08
Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang akitoa neon la ufunguzi kabla ya makabidhiano ya  msaada wa iPad 180 kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Maafisa Mawasiliano Serikalini toka Kampuni ya ving’amuzi ya Startimes, mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Startimes 09Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu You Qing akielezea kufurahishwa na ushirikiano unaondelea kukomaa baina ya Serikali ya Tanzania na China wakati wa sherehe za makabidhiano ya msaada wa iPad 180 kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wenye lengo la  kuboresha utendaji kazi wa Maafisa Mawasiliano Serikalini, msaada huo umetolewa na Kampuni ya ving’amuzi ya StarTimes mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Startimes 10
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Nape Nnauye akitoa shukrani kwa Kampuni ya ving’amuzi ya StarTimes kwa msaada wa iPad 180 wenye lengo la kuboresha utendaji kazi wa Maafisa Mawasiliano Serikalini, mapema hii leo jijini Dar es Salaam.